Tuesday, February 21, 2012

MAANA YA UJASIRIAMALI

Nini maana ya Ujasiriamali?.

Dhana ya Ujasiriamali ina maana pana , miongoni mwa hizo ni;  Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya  katika hali yake ya kiuchumi ambaye ana tabia za kipekee ili kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri) ili awe na hali nzuri zaidi kiuchumi.

Pia katika hali nyingine   Mjasiriamali  anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anajishughulisha mwenyewe(amejiajiri) katika sekta fulani mfano: kilimo, ufugaji au biashara.

Neno Ujasiriamali lina asili ya Kifaransa " Entreprendre" sawa na Kutekeleza/Kufanya shughuli fulani mwenyewe katika uwanja wa kibiashara katika maana rahisi ni sawa na kuanzisha biashara/shughuli ya kujiajiri.

Kwa mitazamo mbalimbali ya wasomi wana muelezea  Mjasiriamali kama mtu ANAYEONGOZA, ANAYEPANGA na ALIYE NA UTAYARI juu ya hatari zozote zinazoweza kujitokeza katika biashara/shughuli yake husika.  

Mchumi wa KiAustrian  Joseph Schumpeter  ameielezea dhana ya ujasiriamali kwa kuegemea mihimili ya UGUNDUZI na UBUNIFU, katika nyanja hizi(yaani kugundua na kubuni):-
-Bidhaa Mpya
-Njia Mpya za uzalishaji/uendeshaji.
-Masoko Mapya
-Mifumo mipya ya Vikundi na Mashirikisho

UTAJIRI unapatikana pindi UGUNDUZI unapoenda sambamba na MAHITAJI, kwa mtazamo huu tunaweza kusema ya kwamba kazi ya Mjasiriamali ni sawa na kuunganisha mbegu za vigezo fulani katika hali ya Ugunduzi na Ubunifu ili kutengeneza ubora na thamani kwa mteja kwa imani ya kwamba thamani itakayopatikana itafidia gharama za mbegu hizo, na hatimaye kutengeneza faida ya kutosha inayopelekea UTAJIRI.

Mpaka hapa tumeweza kumfahamu huyu Mjasiriamali kwa maana na Mitazamo michache. Je kila Mfanya biashara ndogo ndogo ni Mjasiriamali? Tathmini hili kabla hujasoma Article nyingine!

Shukrani kwa kuwa pamoja.


   

9 comments:

  1. Determinants of demand and supply, naomba maelezo juu ya haya mambo namna ambavyo vinaweza kuhusiana na ujasiriamali

    ReplyDelete
    Replies
    1. habari ndugu bura naomba nikujibu swali lako kwa kadiri ya uwezo nitakavyo jaaliwa
      determinants of demand and supply kwa lugha yetu mama niite ni vitu au ni zile sababu ambazo zinapelekea kuongezeka au kupungua kwa uhitaji au usambazaji wa bidhaa au utoaji wa huduma katika eneo husika.
      Katika uhitaji (demand) zipo sababu mfano;-kipato cha muhitaji, alkadhalika katika usambazaji (supply) zipo sababu mfano;- gharama za uzalishaji.
      Haya mambo yana uhusiano mkubwa sana katika biashara yoyote ili kujua zaidi nitafute kupitia facebook ninatumia MOHAK investmet

      Delete
  2. ,wazo zuri ambalo limeniondo kwenye zana potofu ya kwama mjasiliamalin anatakiwa kuwa na mtaji mkubwa

    ReplyDelete
  3. naomba niulize kuna tofauti kati ya mfanya biashara na mjasiria mali

    ReplyDelete
  4. Nikiwa kama kijana ambaye nataka kujiajiri mwenyewe ninatakiwa kuwa na mtaji kiasigani yakuanzia

    ReplyDelete
  5. Habari. Nashukuru sana kwa kunielimisha kuhusu Ujasiriamali.Lakini nina shahuku ya kujua usahihi wa Neno hili: Ujasiriamali au ni Ujasiliamali. Maana nimekuwa nikiona watu tofauti wakiliandika kwa namna hizo mbili tofauti. Pili, natamani kujua Kwanini Hapa Nchini ambako Lugha ya Taifa ni Kiswahili tunaita ENTREPRENEURSHIP kama UJASIRIAMALI/ UJASILIAMALI? Je,Tuliamua kuunganisha MANENO MAWILI: UJASIRI ... NA NENO ... MALI? Pengine kwa kuwa Uanzishaji wa biashara unahitaji Mtu kuwa Imara kukabili MAJANGA? na Kwamba anayefanikiwa kukabili Majanga hayo (Jasiri) ndio atafanikiwa kupata MALI? Nitashukuru kupata Mrejesho toka kwako.
    Davis Binamu, Shinyanga

    ReplyDelete