MWANZO WA BIASHARA KWA MJASIRIAMALI

Mtazamo ni huu

Wateja wengi husikia kwanza jina la biashara au shughuli yako kabla hawajapata habari kamili kuhusu huduma au biashara hiyo. hivyo basi MWANZO ni mmoja na inabidi uanze kwa taswira nzuri.

JINA:
Jina la biashara mathalani linatakiwa liwe Fupi, La Kipekee na Jepesi kukumbukwa, kawaida Mtu huwa na sekunde kama 20 hivi kupata wasaa wa kusikilizwa vizuri na wateja wapya ambao unataka kuwapa habari za shughuli yako, ni vyema jina na maelezo haya ya mwanzo yakawa na sifa za hapo juu ili uanze kuteka hisia za wateja wako. ingawa hakuna njia hasa ya kusema mtu aitumie ili atoe jina zuri la shughuli yake, lakini yampasa kujua umuhimu wake, hasa kwa wakati wa mwanzo.

Kwa haraka tunaweza sema ni vyema mno kama Mjasiriamali anweza tembelea mitandao kama Google(Google It Already) anaweza pata mifano ya aina ya shughuli anayotaka kuifanya na watu wengine wanaofanya shughuli kama hiyo wamefanyaje kwa upande wa majina.

Familia na jamii inayokuzunguka ina nafasi katika hili, unaweza panga mawazo yako, washirikishe wakutathminie mawazo hayo na ikibidi changanua changamoto zao kwani wao ndo watathmini wa awali.

Mamlaka husika kama BRELA,TRA na Halmashauri zinahusika pindi shughuli tunazotaraji kufanya zinaambatana na usajili rasmi kulingana na maeneo yao, suala kama la TIN ni la bure na linaweza pia patikana kwa njia ya mtandao, leseni na makadirio ya TRA ni wastani wa 40,000/= kwa leseni mara moja tu. na 23,500/= TRA kila baada ya miezi mutatu(3).Ni vyema tukatembelea Mamlaka husika kupata taarifa zaidi kama mabadiliko yoyote na utaratibu mwingine.